Thursday, April 22, 2010

: Hakuna mwalimu anayeidai serikali

SERIKALI imesema hadi sasa hakuna mwalimu yeyote anayedai mshahara wala posho ya kujikimu kwa mwaka 2009/2010, Bunge limeelezwa.

Tamko hilo lilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri (TAMISEMI), Agrey Mwanri, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mufindi Kusini, Benito Malangalila (CCM).

Katika swali hilo, Malangalila alitaka kujua ni sababu zipi zinazofanya mishahara ya walimu kucheleweshwa, hatua inayosababisha kero na usumbufu mkubwa hasa kwa walimu wapya wanaoajiriwa.

Akijibu swali hilo, Mwanri alisema baada ya serikali kuanzisha utaratibu mpya ulioanza kutumika Septemba, 2009 mishahara ya walimu wapya inafikishwa vituoni katika mwezi husika ambao mwalimu anapangiwa.

“Aidha wizara yangu imeziagiza halmashauri zote nchini kuwalipa walimu posho ya kujikimu ya siku saba mara tu mwalimu anapofika kuanza kazi. Zoezi hili limefanyika kwa mafanikio makubwa,” alisema.

No comments:

Post a Comment