Thursday, April 1, 2010

Tigo sasa nusu shilingi kwa sekunde

na Mwandishi Wetu


KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo imezindua huduma ya nusu shilingi ambayo itapatikana kwa wateja wate wa Tigo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Uhusiano wa Tigo, Jackson Mmbando, alisema kuwa wateja wote wa Tigo wataweza kufurahia huduma hiyo baada ya dakika ya kwanza ya muda wa maongezi.

“Tigo kama kawaida yetu, leo tunawaletea huduma nyingine nzuri zaidi na lengo ni kumwezesha Mtanzania kupata mawasiliano kwa gharama nafuu kabisa. Sasa mteja wa Tigo ataweza kuzungumza kwa nusu shilingi (thumni) baada ya dakika ya kwanza ya muda wa maongezi,” alisema.

Alisema kwa kufanya hivyo Tigo imerudisha thamani ya thumni katika matumizi ya pesa na kuongeza kuwa huduma hiyo ni ya kudumu.

“Kampuni ya Tigo ndiyo inayoongoza kwa kutoa gharama nafuu kwa watumiaji wake na huduma hii inakuwa ni kwa saa 20 kuanzia saa 12 asubuhi hadi 12 jioni na kuendelea tena saa 4 usiku hadi saa 12 asubuhi,” alisema.

Aliongeza kuwa huduma hiyo ni kwa wateja wa Tanzania Bara na kusema kuwa wateja wao wa visiwani wanaendelea kufaidi huduma ya robo shilingi kwa dakika, ambayo imezinduliwa hivi karibuni visiwani hum

No comments:

Post a Comment